KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 7, 2010

Aua uume wa mumewe baada ya kugundua amezaa nje ya ndoa


AMA kweli waswahili wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi na unavyozidi kusogeza umri unazidi kusikia mengi yatendekao katika hii dunia.
Hivi karibuni mwanaume mmoja [jina kapuni] mkazi wa Mbezi kwa Yusufu amejikuta ameshindwa uzalendo na kutoa siri kubwa iliyokuwa ikimkabili kwa muda mrefu na kuamua kuwaambia ndugu zake wa kiume waliomzidi umri ili waweze kumsaidia sakata hilo.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya ukooo anakotoka mwanaume huyo kilisema kuwa, ndugu huyo aliwatonya ndugu zake kuwa alipokuwa akitoka nje ya ndoa alikuwa hawezi kabisa kushiriki tendo la ndoa na mwanamke ambaye anakuwa nae kwa wakati huo.

Alisema mwanaume huyo alipojaribu tena kuwa na mwanamke mwingine tofauti na yule hali ilikuwa vilevile hakuweza kabisa kushiriki tendo hilo kwa wakati huo kwa kuwa kitendea kazi chake kilikuwa hakihimili kabisa kwa wakati huo

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa mwanaume huyo alipokuwa akimuhitaji mke wake mambo yalikuwa shwari na alikuwa akipafomu kama kawaida jambo ambalo lilimshangaza na lilimuumiza bla mke wake kujua hali hiyo na alikuwa akimuogopa kumuuliza mke wake huyo .

Hali hiyo alidumu nayo kwa takribani miezi saba na aliamua kutupa tena karata kwa mara ya mwisho kwa mwanamke mwingine kujua hali hiyo ilikuwa ikiendelea ama ilikoma.

Bila kuamini kilichomkuta huko ni kilekile kama kilichomkuta kwa wanawake wengine hakuweza kushirikia nae tendo hilo na kupata aibu kubwa kwa wanawake hao.

Ilidaiwa uvumilivu ulimshinda na kuamua kuwaambia ndugu zake wa karibu na nduagu hao kuanza kulifanyia kazi sakata hilo na kuwatafuta dada zao wa makamu wakamuulize mke wa mwanaume huyo alikuwa amemfanyia nini mume wake.

Ilidaiwa awali mwanamke huyo alijing’atang’ata na kutosema ukweli na kudai hakumfanyia chochote na kuwauliza kuwa wao walijuaje kama mume ake hawezi na wakati kwake alikuwa akishirikia tendo hilo kama kawaida.

Kutokana na kibano hicho cha mke huyo walkiamua kutoboa ukweli na kumueleza mume wake akitembea na mwanamke mwingine alikuwa hawezi kushiriki tendo hilo kwa nini?

Bila kuamini mwanamke huyo aliposikia hivyo alicheka na kuwaambia wifi zake hao kuwa “mnaona wenyewe mmekuja kuthibitisha umalaya wa kaka yenu, sa sa ngoja niwaambie nimemkomesha kusudi mana amezidi umalaya”

“Sikieni mimi nimeshazaa watoto watatu hapa yeye likiichomfanya akazae nje ya ndoa nini? Kwa taaria tu nimesikia amezaa na mwanamke mmoja na y eye bado hajanambia

Wamama hao waliinuka mahali hapo na kupeleka ripoti kwa ndugu zao wa kiume kuwa mke wake aliamua kumfanyia hivyo kwa kuwa alizidi umalaya na baada ya jibu hilo wengine alionekana kupandwa na jzba wengine wakimshauri amuache mke huyo kw kuwa hakuwa mwema kwake wengine walismea akamuombe msamaha huku mwenyewe akiwa hana la kusema kutokana na aibu aliyoipata kutoka ka mke wake.

Kwa habari zaidi zitakazoendelea kuhusiana na tukio hilo zitawajia hapahapa.

No comments:

Post a Comment