KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, July 7, 2010

Askari wa kike aliyejipiga risasi aagwa


ASKARI Suzan, aliyejipiga risasi juzi huko Mkoani Mara aliagwa jana na kupewa heshima za mwisho na viongozi wa serikali na kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi.
Askari huyo afisa wa polisi alijipiga risasi juzi kutokana na kutakiwa kujieleza ni kwa nini alikosea kuuongoza msafara wa rais ulikuwa ziarani mkoani humo.

Suzan alikosea kuuongoza msafara wa Rais Kikwete ulipokuwa ziarani wilayani Tarime na kukosea na kuuongoza na kuupeleka njia nyingine ambayo sio husika kwa wakati huo.

Hivyo kufuatia tukio hilo askari huyo alibadilishwa na kupelekwa askari mwingine kwa wakati huo na yeye kutakiwa kujieleza ni kwanini alikosea kuungoza msafara huo na kuuongoza msafara huo wa Rais njia ambayo si husika.

Hivyo kutokana na hali hiyo askari huyo mara baada ya mahojiano hayo aliamua kujipiga risasi na kufariki dunia.

No comments:

Post a Comment