KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 19, 2010

Amnesty International yashutumu Sudan


Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, limeshutumu vyombo vya usalama nchini Sudan kwa kuendesha kampeni za unyanyasaji na vitisho dhidi ya wapinzani wa serikali.

Shirika hilo linasema liliwahoji wafungwa wa zamani ambao wanadai kulikuwa na mateso, kupigwa na kufungwa kinyume cha sheria.

Ripoti hiyo imetolewa siku chache tu baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kutoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa Sudan, Omar Al Bashir kwa kufanya mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.

Rais Bashir amekana mashtaka hayo, na kusema hatambui uhalali wa kisheria wa mahakama hiyo. ICC tayari ilikuwa imetoa kibali kingine cha kukamatwa kwa Rais huyo wa Sudan mwezi Machi mwaka jana kwa makosa ya uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment