KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, July 20, 2010

Afariki Baada ya Kumkodisha Rafiki Yake Ampige Risasi


Mwanaume mmoja nchini Marekani amefariki dunia baada ya dili lake la kumkodisha rafiki yake amjeruhi kwa risasi lilipoenda vibaya.
Kwa mujibu wa polisi wa Dallas nchini Marekani, Ili aweze kupewa umiliki wa mtoto wake aliyenyang'anywa Dwayne Lamont Moten mwenye umri wa miaka 20 alimkodisha rafiki yake ampige risasi ili wamtupie lawama mpenzi wa mke wake kuwa ndiye aliyefanya tukio hilo.

Dwayne alikuwa akiwania mahakamani apewe mtoto wake wa kiume wa miaka mitatu ambaye alichukuliwa na mkewe ambaye hivi sasa anaishi na mwanaume mwingine.

"Hawa ni watu wawili ambao walijaribu kufanya tukio na kumsingizia mtu mwingine", alisema afisa mmoja wa polisi.

Mpango ulikuwa kwamba rafiki yake Dwayne, Jacob Wheeler ambaye naye pia ana umri wa miaka 20, angempiga risasi Dwayne kwa nia ya kumjeruhi tu.

Lakini risasi zilizopigwa zilimjeruhi vibaya sana Dwayne na kupelekea kifo chake.

Polisi walisema kwamba wote wawili Dwayne na Wheeler wana historia ndefu ya makosa ya jinai.

Wheeler amefunguliwa mashtaka ya mauaji na ametupwa jela huku dhamana yake ikiwekwa kuwa ni dola 750,000

No comments:

Post a Comment