KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 17, 2010

Wasomali wafungwa kwa uharamia


Wanaoshukiwa kuwa maharamia wakiwa mahakamani Mei 8, 2010


Mahakama ya Uholanzi imewapa kifungo cha miaka mitano jela Wasomali watano kwa kushambulia meli ya mizigo kwenye ghuba ya Aden mwaka jana, katika kesi ya kwanza ya aina hiyo kusikilizwa barani Ulaya.

Watu hao walishtakiwa mjini Rotterdam kwa kushambulia meli yenye bendera ya visiwa vinavyotawaliwa na Uholanzi, Samanyolu.

Walikamatwa mwaka jana kwenye ghuba ya Aden baada boti yao yenye kasi kubwa kuingiliwa na manowari sindikiza ya Uholanzi.

Maharamia wamejaribu kufanya mashambulia zaidi ya 200 katika pwani ya Somalia mwaka 2009.

'Safari ya uvuvi'
Watu hao watano walikana kuhusika na shambulio hilo kesi hiyo ilipoanza mwezi uliopita, wakisema walikuwa kwenye shughuli zao za uvuvi.

Walikamatwa Januari mwaka jana baada ya kudaiwa kujiandaa kupanda meli hiyo ya Samanyolu, iliyokuwa na mabaharia wa Kituruki.

Jaji amesema amezingatia maisha magumu yaliyopo Somalia yaliyosababisha watu hao kushiriki kwenye uharamia.

Amesema, " Ni bahati tu hakuna aliyeuawa wala kujeruhiwa" katika shambulio hilo

No comments:

Post a Comment