KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, June 17, 2010

Wabunge 3 kufikishwa mahakamani- Kenya
William Ruto
Wabunge watatu akiwemo waziri mmoja wanatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo kujibu mashtaka ya uchochezi.

Wabunge hao walitiwa nguvuni hapo jana na kulala katika kituo cha polisi baada ya kutuhumiwa kutoa matamshi ya kueneza chuki wakati wa kampeni za kupinga raasimu ya katiba mpya inayopendekezwa.

Malalamiko kuhusu wanasiasa hao yalitolewa na tume inayoshughulikia utangamano wa kitaifa nchini humo.

Mwenyekiti wa tume hiyo Mzalendo kibunja, anasema kuwa tume yake haina nguvu ya kuwachukulia hatua wabunge hao na hivyo watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao.

Inaripotiwa kuwa wawili kati yao walitoa matamshi hayo ya uchochezi wakati wa uzinduzi wa makao makuu ya wanaharakati wanaopinga rasimu hiyo ya katiba wiki mbili zilizopita.

Watatu naye anatuhumiwa kuwachochea wakaazi wa eneo lake la ubunge tarehe mosi mwezi huu.

Waziri wa Kilimo William Ruto ambaye anaongoza kundi wa wanasiasa wanaopinga katika hiyo inayopendekezwa anasema, serikali inawalenga ili kuwashurutisha kuunga mkono katiba hiyo.

No comments:

Post a Comment