KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, June 18, 2010

Mwanaume huyu wa nchini Urusi alitaka kuitoa roho yake


Mwanaume huyu wa nchini Urusi alitaka kuitoa roho yake mwenyewe kwa kujirusha toka ghorofa ya tano hadi chini, ilikuwa ni kama sinema wakati baadhi ya watu na polisi walipojaribu kumuokoa.
Mwanaume huyo ambaye jina lake halikupatikana aliamua kujiua mwenyewe kwa kujirusha toka ghorofa ya tano baada ya kupenya dirishani.

Azma yake ilikumbana na vikwazo vya ndugu yake ambao alimdaka mikono kabla hajajirusha.

Kivutio kilikuwa ni bibi aliyekuwa ghorofa ya chini yake ambaye alitumia fagio kumchapa nalo mwanaume huyo aliyetaka kujiua.

Boya lililotandazwa chini na zimamoto liliokoa maisha ya mwanaume huyo wakati alipochoropoka toka ghorofa ya 5 huku akipiga kelele.

Angalia video ya tukio hilo chini

No comments:

Post a Comment