KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Mwanafunzi wa Kike Anapolewa na Kushindwa Kujitambua


KATIKa hali ya kushangaza mwanafunzi mmoja wa kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana, alizidisha unywaji wa pombe hali ambayo ilifanya asiwe anatambua afanyacho kwa wakati huo.
Mwanafunzi huyo alikuwa hajui atendacho eneo la baa alipokuwa akipata kinywaji na wenzake wengine wanne ambao walionekana pombe haikuwachukua na kuzidiwa.

Bila kujitambua mwanafunzi huyo ambaye alijisahau kama alivalia sare za shule alikuwa akifanya vioja katika baa hiyo vitendo ambavyo ni vya kujidhalilisha hali iliyofanya uongozi wa baa hiyo kuwaamrisha wenzake alioongozana nao waondoke mahala hapo ili wamrudishe nyumbani kwao akapumnzike.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi, huko maeneo ya Kariakoo, majira ya jioni ambapo mwanafunzi huyo alishuhudiwa na mwandishi wa habari hii akilazimishwa kuondoka huku yeye akigoma kuondoka mahali walipokuwa wakipata kinywaji hicho.

Nifahamishe ilipojaribu kuzungumza na mmoja wa wanafunzi wenzake waliokuwa na mwanafunzi huyo kutaka kujua kilichomsibu alidai mwenzao huyo alikuwa sio mzoefu wa unywaji wa pombe na kueleza kuwa alikuwa hajanywa bia nyingi na kuhakiki kuwa alikuwa amekunywa bia mbili tu aina ya Savana.

Alidai kabla ya kunywa pombe hizo walimuonya kuwa asinywe kinywaji aina hiyo kwa kuwa hakuwa mzoefu na yeye kuonekana kutaka kufahamu ladha ya kinywaji hicho.

Alidai siku hiyo ilikuwa wanaadhimisha siku ya kuzaliwa ya mwenzao mmoja ambaye yuko kidato cha sita, walikuwa wameandaa siku hiyo ili kumpongeza rafiki yao huyo ambapo walichanga kila mmoja shilingi elfu 30 kusherehekea siku hiyo ambapo walidai ni utaratibu wao kwa marafiki hao watano, mwenzao anapoadhimisha siku ya kuzaliwa huchangishana na kwenda mahala fulani na kuadhimisha siku hiyo.

Wanafunzi hao watano ambao wawili walikuwa ni wa kidato cha sita, wawili kidato cha tano na mmoja alikuwa ni kidato cha nne ambapo wasichana walikuwa watatu na wavulana wawili walimaliza sherehe zao hizo kwa kupata adhabu ya kumbeba mwenzao aliyezidiwa na pombe.

“Lazima tuhakikishe mwenzetu huyu anafika nyumbani kwao salama na sisi ndio twende majumbani kwetu, tunachukua tax hapa sasa hivi tunamrudisha kwao Msasani” walidai.

No comments:

Post a Comment