KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Mbaroni kwa kujifanya afisa wa Takukuru

HISBERT Tijjah, mkazi wa Dar es Salaam, Hisbert Tijjah, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la kujifanya afisa kutoka Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mshitakiwa huyo ilidaiwa alifika katika ofisi za wizara ya Afyana ustawi wa Jamiii na kujitambulisha kuwa yeye ni mkaguzi kutoka taasisi hiyo huku akijua ni udanganyifu.

Akiendesha kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Janeth Ishengoma mbele ya Hakimu Mkazi, Stewart Sanga, alidai kuwa Agosti 7, mwaka 2006, katika ofisi za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii alitenda kosa hilo.

Alifika katika ofisi hizo kwa njia ya udanganyifu na alijitambulisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Brandina Nyoni, na kumueleza kuwa alikuwa na uwezo wa kumsaidia kumaliza tuhuma za rushwa zinazomkabili katibu huyo.

Hata hivyo aligundulika baada ya kufanyika mawasilino na kuchukuliwa hatua.
Ishengoma alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Mshitakiwa alirudi rumande kwa kushindwa masharti ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi serikalini au taasisi inayotambulika.

Pia alitakwia kuwasiisha fedhga taslimu shilingi 100,000 au hati yenye thamani hiyo.

Kesi hiyo itarudi tena Juni 16, mweaka huu, kwa kusikilizwa

No comments:

Post a Comment