KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Masikio ya watanzania Bungeni leo

LEO ni siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na watanzania waliyo wengi kusikia bajeti ya mwaka 2010/11 kutajwa kwa mchakato mzima wa bajeti hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Dodoma leo.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, anatarajiwa kuwasilisha bajeti hiyo kutoa hali halisi ya mapato na matumizi ya taifa kwa mwaka ujao wa fedha.

Bajeti hiyo ya fedha ya trilioni 11 haijulikani itagusa na kuongeza maisha magumu kwa mtanzania wa kawaida kabisa anayeishi kwa mshahara wa kima cha chini ama itampa faraja kwa kupunguza kodi mbalimbali na kuthibiti mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali muhimu

Hata hivyo Waziri Mkulo alipotakiwa na waandishi wa habari kugusia kidogo juu ya bajeti hiyo hakuwa tayari kufafanua na kutia moyo kuwa itakuwa nzuri.

Wakati huohuo bunge hilo limeshatengua kanuni nane muhimu ikiwemo za kupunguza muda wa kuwasilisha bajeti pamoja na kuchangia bajeti kwa wabunge watakaopata fursa hiyo.

Muda wa kuwasilisha bajeti muhimu itakuwa ni wiki tatu badalda ya tano kinyume na ilivyozoeleka kwenye mabunge yaliyopita ya bajeti

Wabunge watakaochangia wamepewa muda wa dakika kumi sio kumi na tano kama ilivyozoeleka awali hii imetokana na bunge hilo kuwa fupi ili kupisha mchakato na shughuli za uchaguzi mkuu ujao

No comments:

Post a Comment