KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 17, 2010

Mapato yatikisa ligi za Ulaya?


Ligi ya mchezo wa soka nchini Ujerumani, inayojulikana kama Bundesliga, imeipita ligi kuu ya England kwa mapato.

Takwimu hizo zimechapishwa katika ripoti mpya ya mapato ya msimu wa mwaka 2008/2009 na shirika la wahasibu, Deloite.

Vilevile ripoti hiyo imeonya kuwa licha ya kupenya kupitia kipindi cha mdororo wa uchumi duniani, bado suala la mishahara ya kupindukia kwa wachezaji linasababisha hofu.

Mchezaji wa club ya Manchester City pamoja na timu ya taifa ya Argentina, Carlos Teves alipoletwa mbele ya waandishi wa habari mwanzoni mwa msimu uliopita alikariri kuwa hakushinikizwa na mapato makubwa ili ajiunge na Manchester City.

Aliyasema hayo wakati akihama kutoka club yenye mapato makubwa Manchester United kwenda Manchester City ambayo licha ya kuwa hakijapata ufanisi kama wa mahasimu wao.

Ripoti hii inahimiza kuwa ni mishahara minono ya wachezaji ambayo huenda ikaviangamiza vilabu.

Usajili wa Tevez ulizidi viwango vya usajili wakati huo. Mshahara wake ulipaa na kufikia dola za kimarekani 218,000 kwa wiki, asilimia 50 zaidi ya mshahara aliyokuwa akiuipokea kutoka club ya Manchester United.

Hata hivyo ligi ya England iliweza kuingiza takriban dola bilioni tatu, kiwango cha juu ikilinganishwa na ligi nyingine duniani, ingawa siyo kwa maana ya faida.

Ligi ya Bundesliga haikufikia kiwango kama hicho lakini ilipata faida.

Hili ni kutokana na kwamba mishahara ya Bundesliga inadhibitiwa kwa kutumia asilimia 51 kwa mishahara ilhali katika ligi ya England asilimia 67 ya mapato hutumiwa kulipa mishahara. Hivyo mapato makubwa bila faida kubwa.

Club ya Manchester City inamilikiwa na Sheikh Mansour, tajiri mwenye mabilioni kutoka ukoo wa ufalme wa Abu Dhabi, na ana uwezo wa kuwalipa wachezaji wake kadri ya mapenzi yake.

Kwa vilabu vidogo shinikizo kubwa lipo la ushindani mfano ni Portsmouth kutoka kusini mwa England.

Msimu uliopita club hii ilizidiwa na kabla ya mwisho wa msimu ilibidi iwekwe chini ya msimamizi ili kuinusuru madeni makubwa kwa wadai pamoja na wachezaji.

Kwa ujumla ni vilabu 13 miongoni mwa vilabu ishirini vya ligi kuu vilivyofanikiwa kupata faida ya matumizi katika msimu uliomalizika wa 2009, kiwango cha chini ukilinganisha na hali ya mwaka mmoja kabla.

No comments:

Post a Comment