KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 17, 2010

Mandela ahudhuria msiba wa Zenani


Nelson Mandela ataonekana hadharani, jambo lililo nadra sana kutokea kwenye msiba wa kitukuu chake Zenani, aliyekufa kwa ajali ya gari wiki iliyopita.

Zenani Mandela, mwenye umri wa miaka 13, alifariki dunia baada ya kutoka kwenye tamasha la Kombe la Dunia mjini Soweto.

Kufuatia msiba huo, Bw Mandela aliahirisha mipango yake ya kuhudhuria ufunguzi wa shindano la Kombe la Dunia.

Dereva wa gari hilo, ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Mandela, alikamatwa na mwanzo kushtakiwa kwa kuendesha akiwa amekunywa pombe, lakini hajafikishwa mahakamani mpaka baada ya Kombe la Dunia kumalizika.

Shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi Bw Mandela, mwenye umri wa miaka 91, alifanya kampeni ili Kombe la Dunia lifanyike Afrika Kusini.

Taswira kupitia televisheni zimemwonyesha akiinuka huku akisaidiwa na mke wake Graca Machel alipokuwa akielekea kwenye benchi la mbele la kanisa dogo lililopo kwenye shule ya Zenani mjini Johannesburg, ambapo msiba huo unapofanyika.

Aliyekuwa mke wa Mandela, Winnie Madikizela-Mandela mama mzazi wa mama yake wa Zenani naye pia alikuwepo, pamoja na viongozi maarufu kwenye nyanja za kisiasa, burudani na michezo na baadhi ya waliosoma nao Zenani.

Kwaya ya nyimbo za injili ya Soweto iliimba wakati wageni walipowasili, baadae wimbo wa miondoko ya Soul ya Bill Wither, Lean on Me ilichezwa huku picha za Zenani zikionyeshwa kwenye skirini.

Shughuli hiyo inatarajiwa kufuatiwa na maziko ya watu wachache.

Zenani alisherehekea siku yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 13 tarehe 9 Juni. Alikuwa miongoni mwa vitukuu tisa wa Bw Mandela.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye rekodi mbaya sana ya usalama wa barabarani, na kuna takriban vifo vya watu 42 kila siku katika barabara ya nchi hizo.

Tamasha la Kombe la Dunia la siku ya Alhamis liliwavutia maelfu ya watu katika uwanja wa Orlando mjini Soweto, huku kukiwa na msongamano mkubwa wa magari mapema Ijumaa.

Tamasha hilo liliwajumuisha wasanii nyota wa kimataifa, akiwemo mwimbaji wa Colombia Shakira, Black Eyed Peas na Alicia Keys, pamoja na wasanii maarufu wa Afrika Amadou & Mariam na Hugh Masekela.

No comments:

Post a Comment