KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Magari ya Rais yaliwekwa mafuta machafu


MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imethibitisha kuwa magari matano yaliyokuwa yakitumika kwenye msafara wa Rais Jakaya Kikwete, katika ziara yake mkoani Kilimanjaro yalijazwa mafuta machafu katika kituo cha TOTAL Rafiki na ndicho chanz
Hayo yalijulikana jana jijini Dar es Salaam, baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha ripoti hiyo kwa vyombo vya habari.

Akizungumza na wanahabari hao, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw.Haruna Masebu, alisema mamlaka hiyo imethibitisha mchezo mchafu huo baada ya uchunguzi wa kina wa kimaabara uliofanywa na kubaini mafuta yaliyojazwa kwenye magari hayo yalikuwa machafu.

Alisema mara baada ya mamlaka hiyo, kupokea taarifa za magari ya Ikulu kuwekewa mafuta hayo walisimamisha na kutoa maelezo kuwa gari lililoshusha mafuta hayo kwenye kituo hicho liwekwe chini ya ulinzi na lisiondoke mahali hapo na walifika kuchukua sampuli ya mafuta hayo.
Hivyo uchunguzi ulibaini kuwa mafuta hayo hayakuwa mazuri kama ipasavyo.

Hivyo kutokana na tukio hilo mamlaka hiyo imetoa siku saba kwa wamiliki wa vituo hivyo kujitetea kabla ya kuchukuliwa hatua kali na stahiki kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo alisema mamlaka hiyo iliwapa adhabu ya kuwafungia vituo hivyo kutofanya shughuli hizo za uuzaji mafuta kwa kipindi cha mwaka mmoja na kulipa faini ya shilingi milioni 25 na kituo cha Maunt Meru Petroleum Ltd-Uchira ambacho kinauza mafuta ya jumla kitatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 100.

No comments:

Post a Comment