KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Mabasi ya wanafunzi yazinduliwa Dar


JANA Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizindua mradi wa mabasi ya kubebea wanafunzi jijini Dar es Salaam yaliyotolewa na benki ya CRDB.
Mabasi hayo matano yenye thamani ya shilingi milioni 500 yametolewa na benki hiyo kwa lengo la kusafirishia wanafunzi nyakati za asubuhi na jioni wakati wanafunzi hao wanapata misukosuko na usafiri..

KAtika hotuba aliyoitoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema kuwa kuna uhitaji wa mabasi elfu kumi zaidi ya kusafirishia wanafunzi yanahitajika.

Alisema baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa Jiji la Dar es Salaam lina wanafunzi zaidi ya 550,000 wanaohitaji usafiri wa kwenda na kurudi shuleni kila siku ambapo kero ya usafiri inawaathiri kwa kiasi kikubwa.

Aliwapongeza viongozi wa Benki ya CRDB kubuni mradi huo wa mabasi kwa uona adha zinazowakabili wanafunzi na kuwataka wahisani wengine kujitokeza na kuiga mfano huo kwa kwua kuna uhitaji zaidi ya mabasi ya wanafunzi

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei alisema mradi huo, umelenga kutatua changamoto wanazozipata wanafunzi, ikiwa ni moja ya mipango ya kuisaidia jamii ndani ya benki hiyo.

Hata hivyo mradi huo utakuwa chini ya UDA kwa kuwa wameona wao wana uwezo mkubwa wa kutumia huduma hiyo ya usafirishaji nchini

No comments:

Post a Comment