KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 17, 2010

..Kuna ukame wa magoli Afrika Kusini?


Mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA yakiwa yameingia wiki ya pili nchini Afrika Kusini, inaalezwa yameingia katika historia ya kufungwa mabao machache hadi sasa.

Ikiwa imekwishachezwa michezo 15 yamefungwa mabao 23 tu, ikiwa ni rekodi, kwani michezo yote iliyopita nyakati kama hizi milango ilikuwa imekwishafunguliwa shabaha
Hata pamoja na kutengenezwa mipira mipya aina ya Jabulani, iliyoundwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, Fifa ikiwa na lengo la kuwezesha makipa kupata shida kukamata mikwaju (kama ilivyomtokea Robert Green kipa wa England na Faouzi Chouchi wa Algeria), bado washambuliaji wamekuwa butu katika michuano hii ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Ingawa inaweza kuwa ni mapema mno kusema mashindano yamekosa magoli, huenda wachezaji wakishazoea hali ya hewa ya Afrika Kusini na mpira wenyewe, tutaanza kushuhudia michomo ikiingia nyavuni.

Timu za Afrika

Baada ya kushuhudia timu za Afrika zikiteleza katika mechi zao za kwanza katika Kombe la Dunia, ama kupoteza michezo au kwenda sare na timu moja tu Ghana ikiweza kushinda mchezo wake wa ufunguzi, bado kuna tamaa Afrika inaweza kufanya vyema katika mechi zinazofuata.

Walikuwa wenyeji Bafana Bafana walioanza kufungua pazia tarehe 11 Juni, walipotoka sare na Mexico timu inayoelezwa si kali sana katika kundi A ikilinganishwa na Uruguay pamoja na Ufaransa.

Bado wenyeji wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele hasa kutokana na maneno yao wenyewe, wamekwishaondoa hofu ya kushiriki Kombe la Dunia wakiwa wenyeji.

Je baada ya Brazil kukaliwa kooni na Korea Kaskazini hadi kulazimika kupata mabao mawili katika kipindi cha pili, Brazil imelichepusha Kombe la Dunia kwa samba iliyotarajiwa?

Mabingwa watetezi Italia nao baada ya kubanwa mbavu na Honduras kuna tamaa ya kutetea taji lao licha ya historia kuonesha hakuna nchi iliyowahi kushinda Kombe la Dunia mara mbili mfululizo, haya ruksa tunakaribisha maoni yako.

No comments:

Post a Comment