KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, June 20, 2010

Familia ya Watu 162 Inayoishi Nyumba Moja


Hii huenda ikawa ndio familia kubwa kuliko zote duniani inayoishi nyumba moja. Mwanaume mwenye wake 38 na watoto 94 na wajukuu zake wote kwa pamoja wanaishi nyumba moja.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 66 aliyejulikana kwa jina la Ziona, huenda akawa ndio kiongozi wa familia kubwa kuliko zote duniani inayoishi nyumba moja.

Ziona mwenye wake 38, anaishi pamoja na wake zake wote pamoja na watoto wake 94 na wajukuu zake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times of India, familia hiyo kubwa ipo kwenye mji wa Mizoram, mashariki mwa India.

Familia hiyo kubwa hutumia jiko moja kupika msosi kwaajili ya familia nzima.

"Kila siku tunapika kilo 50 za mchele kwaajili ya chakula cha jioni, tunapotaka kula nyama huwa tunapika kilo 30-35 za nyama ya nguruwe", mke mmoja wa Ziona aliliambia gazeti hilo

No comments:

Post a Comment