KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

CCJ wajipanga kuandamana

CHAMA Cha Jamii (CCJ) kipo katika maandalizi ya kufanya maandamano ya amani kwa wanachama wake ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kwenda katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa ili kupinga kauli iliyodaiwa hakijatimiza masharti stahili
Nia ya maandamano hayo ni kutaka kumdhihirishia msajili huyo kuwa idadi ya wanachama wanaotakiwa ili wapewe uhakiki wametimia ambapo awali walishindwa kusajiliwa kwa kuwa msajili huyo alidai ndani ya mkoa wa Dar es Salaam kuna wanachama wapatao 13 tu.

Katibu Mwenezi Taifa wa CCJ, Constantine Kitanda aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandamano hayo yana lengo la kuuthibitishia umma wanavyopigwa danadana juu ya usajili wa chama hicho ili wasishiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema wanahakikisha katika maandamano hayo wanachama hao wapatao 200 watabeba na kadi zao na vitambulisho kuwa ni wanachama wa chama hicho.

“Kauli ya Tendwa ya kusema kuwa CCJ ina wanachama 13 mkoa wa Dar es Salaam ni uongo uliopitiliza kwa kuwa upande wa viongozi tu wapo 25 baki wanachama wao ambao ni zaidi ya 200” alisema.

Alisema endapo watanyimwa usajili huo ili hali wanachama watafika na kadi zao basi wataitisha maandamano nchi nzima kupinga vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment