KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, June 21, 2010

Cameroon yatolewa Kombe la Dunia


Cameroon wamekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano ya Kombe la Dunia 2010.

Camerooon imekuwa timu ya kwanza kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini baada ya kushindwa mabao 2-1 na Denmark mjini Pretoria.

Cameroon ndiyo waliotangulia kufunga katika dakika ya 10 kupitia nahodha wao Samuel Eto'o, akimalizia pasi ya Achille Webo.

Matatizo
Katika dakika ya 33, Nicklas Bendtner, aliisawazishia Denmark baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Simon Kjaer.

Bao la ushindi la Denmark lilifungwa katika dakika ya 61 na Dennis Rommedahl baada ya kumzidi kasi Jean Makoun kutokea upande wa kulia wa uwanja.

Indomitable Lions bado wana mechi moja iliyosalia dhidi ya Uholanzi ambayo tayari imekwishafuzu kwa raundi ya pili, na hata ushindi katika mechi hiyo hautaiwezesha Cameroon kusonga mbele.

Nafasi ya pili ya kufuzu miongoni mwa 16 bora kutoka kundi E itang'ang'aniwa na Denmark na Japan, Alhamisi ijayo, timu hizo mbili zimekwishaifunga Cameroon.

Uholanzi ilifuzu mapema Jumamosi baada ya kuifunga Japan bao 1-0.

This content requires Flash Player version 10 (installed version: No Flash Flayer installed, or version is pre 6.0.0

No comments:

Post a Comment