KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, June 17, 2010

Cameron aiomba radhi Ireland


Tume iliyochunguza mauaji ya waumini 13 wa kanisa Katoliki yaliyofanywa na wanajeshi wa Uingereza mwaka 1972 imebaini kuwa wanajeshi hao hawakuwa na haki kuwafyatulia risasi waumini hao.

Uchunguzi wa tukio hilo lililojulikana kama Bloody Sunday umeonyesha kuwa mmoja wa watu waliouawa alikuwa tishio.

Akitangaza matokeo ya uchunguzi huo katika bunge la Uingereza waziri mkuu David Cameron amesema watu waliouawa au kujeruhiwa walikuwa wakikimbia eneo la tukio au kuwasaidia wenzao.

Na hakuna hata mmoja aliyekuwa na silaha au kuhatarisha maisha ya wanajeshi.

Cameron aliomba radhi kwa niaba ya serikali na taifa akisema wanajeshi hawakutoa onyo lolote na baadae walisema uwongo kuhusu kilichotokea.

Ripoti hiyo imetolewa baada ya uchunguzi uliodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.

Familia za marehemu zilifurahia uamuzi huo wakisema wamesubiri kwa miongo kadhaa kupata ukweli.

Baadhi yao walirarua nakala za ripoti ya uchunguzi wa awali ambayo ilisema jeshi la Uingereza halikuwa na hatia yoyote

No comments:

Post a Comment