KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 12, 2010

Afrika Kusini yalazimisha sare na Mexico

Wenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini, wameanza michuano hiyo kwa matumaini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mexico.

Mexico wenye uzoefu mkubwa wa kucheza katika Kombe la Dunia walianza kwa kumiliki mpira kwa kipindi kirefu, lakini walishindwa kumalizia nafasi zilizopatikana.

Baada ya mapumziko, kocha wa Afrika Kusini, Carlos Alberto Parreira, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Lucas Thwala na kumwingiza Tsepo Masilela.

Piga nikupige

Mabadiliko hayo yalizaa matunda wakati Siphiwe Tshabalala, kiungo wa Kaizer Chiefs, alipotikisa nyavu katika dakika ya 55 kuipatia Afrika Kusini goli la kuongoza.

Goli hilo lilishangiliwa kwa mbwembwe zote zilizoambatana na dansi kavu kavu wakati wachezaji walipokusanyika pembeni.

Bahati mbaya kwa Afrika Kusini, kosa la kushindwa kuwakaba wachezaji wa Mexico katika eneo la hatari lilitoa fursa kwa Rafael Marques kusawazisha katika dakika ya 79.

No comments:

Post a Comment