KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, May 22, 2010

Zain yaja na Balckberry Pre Paid

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zain Tanzania imezindua huduma mpya itakayojulikana kwa Blackberry Pre Paid.
Uzinduzi huo umefanywa na Meneja Mawasiliano wa Zain Beatrice Singano Mallya leo jijini Dar es Salaam.

Alisema huduma hiyo ya Blackberry Pre Paid ni huduma ambayo itonufaisha wateja wa mtandao huo nchini kote.

Singino alisema Zain imezindua huduma hiyo ikiwa ni katika mwendelezo wake wa kuboresha huduma zake hapa nchini pamoja na kuwatimizia mahitaji wateja wake.

"Leo hii najisikia furaha katika kupanua huduma zetu hasa kwa wateja wetu wa Pre Paid kwa huduma zitaboreka zaidi," alisema Singano.

Alisema kwa wateja ambao watahitaji kujiungana huduma hiyo watahitajika kutoa shilingi 35,000 kwa mwezi.

Singano alisema huduma hiyo itahusu wafanyabiashara na wateja wa kawaida ambapo wateja watakao jiunga kabla ya Aprili 30 watapata mwezi mmoja bure.

Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Kevin Twisa alisema kampuni hiyo imetangaza promosheni nyingine ya kusugua na ushinde ambayo itaongeza mamilionea kuzunguka nchi nzima.Alisema promesheni hiyo itakuwa inamapatia mteja mmoja shilingi milioni 10 kila wiki ambapo promosheni hiyo itakuwa ya miezi miwili.

Alisema mshindi wa pili atajishindia muda wa maongezi wa shilingi 100,000 ana washindi wengine 50 ambao watashindwa watajishindia muda wa maongezi wa shilingi 10,000.

No comments:

Post a Comment