KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 15, 2010

Wanafunzu wanatafutwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mlinzi wa chuoni hapo.


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua) cha mjini Morogoro Campas ya Mazimbu, wanatafutwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mlinzi wa chuoni hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, alisema tukio hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu, saa 12 jioni, maeneo ya chuo hicho.

Alimtaja mlinzi huyo kuwa ni Japhari Thabiti kutoka kampuni ya Moku Security ya mjini hapa (38), mkazi wa Chamwino, Manispaa ya Morogoro.

Alisema wanafunzi hao wanaokadiriwa kuwa kati ya watano na sita, inadaiwa walimpiga mlinzi huyo sehemu za kichwani pamoja na maeneo mbalimbali ya mwili hali iliyopelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Alisema hata hivyo, mlinzi huyo alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo na kwamba mwili wake unasubiri kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.

Andengenye alisema chanzo cha kifo hicho kilitokana na ugomvi uliosababishwa na upotevu wa simu ya kiganjani katika bweni la wasichana na hivyo wanafunzi hao kuchukua jukumu la kutoa kichapo kwa mlinzi huyo kwa madai ya kuwa yeye anafahamu mwizi wa simu hiyo.

Wakati huo huo, mtoto mwenye umri wa miaka (6), Japhet John, mkazi wa Ifakara Wilaya ya Kilombero, amekutwa amekufa porini wakati akichunga ng’ombe.

Kamanda Andengenye alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi, maeneo ya Ifakara.

No comments:

Post a Comment