KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 13, 2010

Walienda Kwenye Daraja Kujiua Lakini...


Walienda kwenye daraja kwa nia ya kujirusha kila mmoja akiwa na sababu zake mwenyewe za kuhitimisha maisha yake lakini bila kutarajia badala ya kujiua waliangukia kwenye mapenzi na hivi sasa wanategemea kuoana.
Andriej Ivanov, 26, wa nchini Urusi alienda kwenye daraja la mji wa Ufa katikati mwa Urusi kwa nia ya kujirusha ili afariki.

Ivanov aliamua kujiua baada ya mchumba wake kufariki siku moja kabla ya harusi.

Lakini Ivanov alipofika kwenye daraja hilo alimkuta mwanamke aliyejulikana kwa jina la Maria Petrova, 21, akiwa anang'inia kwenye machuma ya daraja akiwa tayari kujirusha ili ajiue.

Maria kwa upande wake aliamua kujiua baada ya wazazi wake kumfukuza nyumbani kwao alipopata ujauzito kabla ya kuolewa.

Ivanov alipomuona Maria anajiandaa kujirusha darajani, aliamua kuingilia kati na kuanza kumsihi asijiue.

"Kuna hisia zilinijia na sikutaka kumwachia Maria ajiue ingawa mimi mwenyewe nilikuwa na masaibu yangu yaliyonivunja moyo", alisema.

"Alibadili uamuzi wake wa kujiua, alilala mikononi mwangu huku akilia sana, nami ndipo nilipoanza kulia pia".

Ivanov aliezea jinsi walivyotumia siku hiyo pamoja wakipiga stori mpaka asubuhi na kuahidiana kusaidiana kupeana moyo baada ya masaibu yaliyowakuta.

Ivanov na Maria waligeuka kuwa wapenzi baada ya siku hiyo na hivi sasa wanapanga kufunga ndoa.

No comments:

Post a Comment