KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, May 22, 2010

Wakulima wa embe wasaidiwa milioni 126/-

MFUKO wa Maendeleo ya Afrika (ADF) umetoa msada wa shilingi milioni 126 kwa Chama cha Wakulima wa Embe (AMAGRO) katika mikoa ya Tanga, Dar es Salam na Pwani.
Fedha hizo zilizotolewa na serikali ya Marekani, zinalenga kuimarisha uwezo wa chama hicho.

AMAGRO imekuwa ikihamasisha kilimo cha embe kwa ajili ya uchumi endelevu wa taifa.

Kulingana na taarifa ya Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam, msaada huo utawanufaisha wakulima wadogo 65 wa zao hilo kwa ajili ya kuzalisha embe bora na kuuza nje ya nchi.

Lengo lingine la msaada huo ni kuiwezesha AMAGRO kuwa mzalishji wa embe zenye ubora wa kimataifa pamoja na mamzao mengine ya embe katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Tarifa hiyo ilieleza kuwa, msaada huo wa ADF utawasaidia wakulima wa embe kuanzisha mashamba ya mfano, kuwafundisha wafanyakazi na wakulima masuala ya uongozi, mifumo ya fedha, uendelezaji wa mipango ya biashara na mbinu z utafutaji wa masoko.

ADF ambalo ni shirika la serikali ya Marekani limekuwa likidhamiria kufungua fursa za kiuchumi barani Afrika.

Kwa sasa ADF inafanya kazi zake katika zaidi ya nchi ya 20 barani Afrika ambapo kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita Shirika hilo limefadhili karibu miradi 1,500.

Kwa sasa shirika hilo linafadhili miradi 27 ya uwekezaji nchini yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2 ambapo hapa nchini shirika hilo limekuwa likifadhili miradi ya kiuchumi tangu mwaka 1986.

Katika hatua nyingine shirika hilo limetoa msaada kwa wakulima wa kakao wa Mbingu wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Wakulima hao wamepatiwa msaada wa dola za Marekani 99,000 kwa ajili ya kuwajengea wa uwezo wakulima wa zao hilo kupitia chama cvha wakulima wa Kakao Mbingu (MOCOA).

Msaada huo unalenga kuwawezesha wakulima hao kuendesha kilimo hai cha zao hilo kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment