KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 13, 2010

Vijana wa Kibongo wachomwa moto A.Kusini

2008-04-11 17:46:58
Na Francisca Jeremiah, Jijini


Vijana wawili wa Kitanzania imedaiwa wamepoteza maisha baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kulipuliwa na petroli kutokana na bifu la wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea hivi karibuni huko Afrika ya Kusini.

Habari zimewataja vijana wanaodaiwa kuuawa kuwa ni Mohamed Kambangwa,18 na mwenzake Abdallah Gea, 20.

Kaka wa marehemu Mohamed, aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Kambangwa, amedai kuwa mdogo wake aliuawa na kijana wa Kizungu kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa akimchukulia mkewe.

Imedaiwa kuwa Mzungu huyo alimwagia petroli nyumba ambayo Watanzania hao walikuwa wamelala.

Bw. Abdallah amesema miili ya marehemu italetwa nchini kesho kwa mazishi. Amesema kwa hapa Bongo, familia za marehemu zinaishi katika maeneo ya Tandika mtaa wa Sambwisi.

Habari zaidi zimedai kuwa mtuhumiwa ametiwa mbaroni na vyombo vya dola kwa hatua zaidi za kisheria.

SOURCE: Alasiri

No comments:

Post a Comment