KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, May 21, 2010

Uturuki yaisaidia Somalia


Uturuki imesema inafanya mkutano wa kuijenga upya Somalia kama jitihada zake za kupanua wigo wa kibiashara na kidiplomasia duniani.

Mkutano huu unaodhaminiwa na Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia unafanyika katika muhula wa Uturuki kama mwanachama asiye wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa..

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje Burak Ozugergin hii ni sehemu ya mkakati mkubwa zaidi wa kuimarisha mshikamano na mataifa ya Afrika.

Amesema wamefungua ofisi tano za kibalozi barani humo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, na wanakusudia kuongeza idadi hiyo maradufu katika kipindi cha mwaka huu pekee.

Umoja wa mataifa na nchi za Magharibi watautumia mkutano huu kuonyesha uungaji wao mkono kwa serikali iliyoelemewa ya Somalia ambayo inadhibiti eneo dogo tu linalozingirwa na wanaharakati wa kiislamu.

Msimamo wa Uturuki ni kuhimiza mazungumzo na ukarabati lakini pia likiwa taifa kuu linalotumia bahari katika kuendesha biashara yake ya kimataifa.

Vile vile ina wasiwasi kuhusu uharamia wa baharini katika mwambao wa Somalia.

Hivi sasa meli moja ya Uturuki inazuiliwa na maharamia na inachangia katika kikosi cha kimataifa kinachopambana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment