KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 10, 2010

Uchaguzi mkuu wafanyika Ufilipino


Shughuli ya kupiga kura za urais na maeneo imeanza nchini Ufilipino huku kumiwa na milolongo mirefu ya wapiga kura.

Raia wa Ufilipino wanamchagua rais, naibu rais pamoja na kujaza nyathifa nyingine 17,000 za wajumbe.

Muda wa kupiga kura umeongezewa kwa saa moja, huku wapiga kura wakilazimika kukaa saa nyingi kwa milolongo kutokana na kuwepo kwa mashini mpya zinazotumiwa kuhesabu kura. Baadhi ya mashini zimeripotiwa kuharibika.

Huku haya yakiarifiwa watu sita wameuawa wakati shughuli hiyo ikianza katika eneo la kusini ambapo kumekuwa na machafuko ya kisiasa.

Bengno Aquino mwanawe aliyekuwa rais, Cory Aquino anaongoza katika kura ya maoni ya urais na anakabiliwa na upinzani kutoka kwa rais wa zamani Joseph Estrada na bilionea Manny Villar.

Rais anayeondoka Gloria Arroyo ambaye muhula wake unamazilika mwezi Juni anawania kiti cha ubunge.

No comments:

Post a Comment