KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, May 10, 2010

Taliban 'inahusika' na bomu New York


Marekani imedai kuwa na ushahidi unaoonyesha kuwa kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Pakistan ndiyo lilihusika na jaribio la kulipua bomu la kutegwa garini ambalo halikufanikiwa katika viwanja wa Times jijini New York hivi karibuni.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Eric Holder, alitoa maelezo hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha "This Week" kinachorushwa na televisheni ya ABC.

Awali maafisa wa Marekani walikana madai ya kundi hilo kuhusika na njama hiyo katika mojawapo ya mitaa inayokuwa na idadi kubwa mjini New York.

Raia wa Marekani mzaliwa wa Pakistani ameshafunguliwa mashtaka ya kujaribu kulipua eneo linalovutia wataalii wengi, tukio lililotokea juma moja lililopita.

No comments:

Post a Comment