KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 15, 2010

Sudan yadhibiti ngome ya waasi Darfur


Jeshi la Sudan limesema limefanikiwa kudhibiti ngome moja iliyokuwa ikishikiliwa na waasi katika jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi, Al-Sawarmi Khaled, ameeleza kuwa zaidi ya waasi 100 kutoka kundi la Justice and Equality Movement (Jem) waliuawa katika eneo la Jebel Moon.

Waasi hao wanasema waliondoka mwezi uliopita kuepusha vifo vya raia.

Waasi hao walisaini makubaliano ya awali ya amani na kusitisha mapigano mwezi Februari huko Khartoum, lakini baadaye walijitoa kwa madai kuwa serikali ilikuwa ikijihusisha na vitendo vya vita.

Mwandishi wa BBC, James Copnall, aliyeko mji mkuu Khartoum, anasema mgogoro wa Darfur ulilipuka upya majuma kadhaa yaliyopita baada ya kutulia katika miaka ya karibuni.

Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika hali ya Darfur huku waasi wakionekana kugawanyika katika makundi madogo kwenye maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na jimbo la jirani Kordofan, kwa mujibu wa mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment