KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 22, 2010

Soko la samaki laingiza bilioni mbili

SOKO la Kimataifa la samaki Feri Dar es Salaam limeingiza shilingi bilioni 2.2 mwaka jana.
Kiasi hicho cha fedha kimepatikana kutokana na mauzo ya kilo zaidi ya milioni 2.3 zilizouzwa katika kipindi hicho.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Afisa uvuvi katika soko la Feri Mwajuma Moyo alisema Samaki ni wale waliovuliwa katika bahari ya Hindi.

Moyo alisema jumla ya aina 42 za samaki waliouzwa sokoni hapo wakiwemo Antepa, Chaa, Changu, Chewa, Chuchunge, Dagaa na vibua.

Alisema wateja wakubwa wa samaki hao ni wafanya biashara wadogo wanaonunua kwa jumla na kwenda kuuza reja reja.

Kuhusu mauzo ya samaki afisa uvuvi huyo alisema hutegemea na msimu na aina ya samaki ambapo alitolea mfano wa dagaa ambao huuzwa kati ya shilingi 650 kwa ndoo ya kilo 20 hadi shilingi 12,000 lakini hutegemea msimu.

Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa soko hilo Hamza Hassan alisema mbali na kupatikana kwa samaki hao pia Tani 900 samaki huingizwa sokoni hapo kutoka Tanga, Mafia na Kilwa.

Alisema tani 30 huingia kutoka nje ya nchi ambapo walaji wakubwa wa samaki ni wakazi wa Dar es saal, mikoa ya Pwani na mikoa jirani ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment