KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 22, 2010

Rais Köhler afanya ziara Afghanistan

Rais wa Ujerumani Horst Köhler leo amefanya ziara ya ghafla isiyotarajiwa nchini Afghanistan, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Ujerumani kuizuru nchi hiyo katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.
Mara ya mwisho kwa rais wa Ujerumani kuitembelea Afghanistan ilikuwa mwaka 1976 wakati huo rais akiwa Heinrich Lübke.

Rais Köhler akiongozana na mkewe Eva Luise aliwasili katika kambi ya wanajeshi wa Ujerumani kwenye mji wa Mazar-i-Sharif kaskazini mwa Afghanistan. Ziara ya Rais Köhler haikutangazwa kutokana na sababu za kiusalama.Aliwasili akitokea Shanghai China alikotembelea maonesho ya biashara duniani.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Majeshi ya Ujerumani katika mji wa Masar-i-Scharif kaskazini mwa Afghanistan Katika ziara yake hiyo Kiongozi huyo wa taifa amewaambia wanajeshi wa Ujerumani kuwa, nchi yao inawaungaa mkono katika jukumu wanazofanya kuisaidia na kuijenga Afghanistan.




Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed

No comments:

Post a Comment