KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, May 22, 2010

Nani Mbabe Kati ya Bayern Munich na Inter Milan ?

Mtanange wa fainali ya klabu bingwa ulaya unafanyika leo usiku kwa kuwakutanisha mabingwa wa Italia, Inter Milan na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.
Ni muda mfupi umebaki kabla ya bingwa mpya wa ulaya kujulikana.

Inter Milan ikiongozwa na kocha wao Jose Mourinho inapewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe lakini vijana wa Louis van Gaal wako kamili kuweka rekodi ya kulitwaa kombe kwa mara ya nne.

Inter Milan itaingia uwanjani bila ya Thiago Motta ambaye alipewa kadi nyekundu mechi iliyopita na Barcelona.

Nahodha wa Inter, Javier Zanetti atacheza kwenye nafasi ya kiungo huku Cristian Chivu akirudi nyuma kucheza beki nafasi ya Zanetti.

Lucio ambaye yuko fiti tena atarudi uwanjani kwenye fomesheni ya Inter ya 4-2-3-1 ambapo Samuel Eto'o, Goran Pandev na Wesley Sneijder watakuwa nyuma ya Diego Milito katika safu ya ushambuliaji.

Bayern Munich kwa upande wao watamkosa winga wao Franck Ribery ambaye anaendelea kutumikia adhabu ya mechi tatu kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kwenye mechi ya nusu fainali.

Hata hivyo, Muargentina, Martin Demichelis amerudi ufiti wake na kocha wa Bayern hatasita kumuingiza kwenye kikosi chake cha kwanza kitakachoshuka dimbani.

Mechi ya fainali inachezwa kwenye uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu kuanzia saa nne kasoro kwa saa za Tanzania.

No comments:

Post a Comment