KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 10, 2010

Nani alitaka kulipua bomu Marekani?


Wachunguzi nchini Marekani wanachambua vidhibiti kadhaa kupata vidokezo watu au kundi gani lilihusika na njama ya kutega bomu katika viwanja vya Times mjini New York, eneo ambalo ni maarufu kwa shughuli za burudani.

Bomu hilo lililoelezewa "kuwa si la kitaalam", lilikuwa na mitungi ya gesi aina ya propane, fashi fashi, mafuta ya petroli na saa. Bomu hilo lilitegwa ndani ya gari aina ya Nissan Pathfinder.

Kamishna wa polisi wa New York, Ray Kelly, amesema hapakuwa na ushahidi kuonyesha kuwa kundi la Taliban lilihusika na jaribio hilo.

Je, Taliban wanahusika?

Mapema Jumapili kundi la Taliban la Pakistan lilijigamba kuhusika.

Katika ujumbe wa video unaodaiwa kutolewa na Pakistani Taliban, wanamgambo hao walisema walikusudia kulipiza kisasi vifo vya kiongozi wao na kiongozi wa Al Qaida nchini Iraq.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili, Bw Kelly alisema bomu hilo lilikuwa limeunganishwa na vifaa viwili vya kuhesabia muda kwa waya kuingia kwenye kopo, ambalo wanaamini ndiyo kilipua bomu, matanki ya gesi ya propane na kasha la bunduki.

Bw Kelly pia amesema mtu mmoja mwenye asili ya kizungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka ya 40, alionekana akiondoa shati jeusi katika eneo hilo na kuliweka kwenye mkoba.

No comments:

Post a Comment