KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 3, 2010

Mtambo wa kuchimbia mafuta ujulikanao kama Deepwater Horizon, ulizama tarehe 22 Aprili, na kusababisha kuvuja kwa mafuta hayo.

Obama atembelea eneo yanakovuja mafuta
Rais Barack Obama wa Marekani ameelezea kuvuja kwa mafuta katika Ghuba ya Mexico ni janga kubwa la kimazingira ambalo halijawahi kutokea.

Akizungumza huko Louisiana, Bw Obama alisema serikali yake itafanya kila linalowezekana kuondoa mafuta hayo, na kuongeza kuwa BP inahusika na kuwajibika kwa gharama za usafishaji wa mazingira.

Alisema kazi ya muhimu kwa sasa ni kuzuia mafuta yasisambae zaidi katika pwani ya Ghuba.

BP inasema itachukua zaidi ya wiki moja kabla ya mipango ya dharura kuzuia uvujaji huo haijaanza kuzaa matunda.
Lakini huenda kazi ya kuchimba visima vya pembeni kusaidia kunyonya mafuta ikamalizika baada ya miezi kadhaa kumaliza kabisa tatizo hilo, Waziri wa mambo ya ndani, Ken Salazar alionya siku ya Jumapili.

Mtambo unaoendeshwa na BP wa kuchimbia mafuta ujulikanao kama Deepwater Horizon, ulizama tarehe 22 Aprili, siku mbili baada ya mlipuko kuua watu 11.

Athari za kiuchumi na mazingira

Gavana wa Louisiana, Bobby Jindal, ameonya kuwa mafuta hayo yanahatarisha uhai wa jimbo lake.

Bw Obama alisafiri kwenda Louisiana siku ya Jumapili kujionea mwenyewe uharibifu huo.

Akizungumza kutoka mji wa Venice, alisema: "Tunakabiliana na janga kubwa la mazingira na huenda halijawahi kutokea awali.

"Mafuta yanayovuja kutoka kwenye kisima yanaweza kuathiri vibaya uchumi na mazingira ya majimbo yetu ya Ghuba ya Mexico.

"Na huenda likachukua muda mrefu. Linaweza kuhatarisha shughuli za maelfu ya wamarekani wanaoshi maeneo haya."

No comments:

Post a Comment