KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 19, 2010

Mataifa yakubali vikwazo dhidi ya Iran

Marekani, Urusi na China, zimeafiki azimio la Umoja wa Mataifa linalotaka vikwazo zaidi kwa Iran, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton,


Nyuklia Iran

Akizungumza mbele ya kamati ya seneta ya uhusiano wa nje, Bi Clinton amesema azimio hilo litasambazwa miongoni mwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili lipate idhini.

Kauli hiyo ya Hilary Clinton ameitoa siku moja tu baada ya Iran kufikia makubaliano na Uturuki ambapo nchi hizo zitabadilishana madini ya uranium yaliyorutubishwa kwa nyenzo za nguvu za nyuklia.



Iran itaikabidhi nchi hiyo nyenzo zake za nyuklia.

Mkataba huo ulikuwa kama ule uliopendekezwa na nchi za magharibi na washirika wao mwaka uliopita.


Iran itakabidhi nyenzo zake za nyuklia kwa Uturuki.
Lakini makubalino na Uturuki hayakuchangamkiwa na Marekani na washirika wake.

Siku ya Jumanne Bi Clinton alisema bado kulikuwa na maswala kadhaa yaliyohitaji jawabu.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliyahimiza mataifa duniani kuunga mkono mkataba wake na Iran na ikiwa nchi hiyo haitasafirisha madini ya uranium katika kipindi cha mwezi mmoja kama walivyokubaliana basi itajikuta peke yake.

No comments:

Post a Comment