KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 20, 2010

Mashindano ya Kuchora Katuni za Mtume Yasababisha Mzozo


Mashindano ya kuchora katuni za mtume Muhammad (S.a.w) ambayo yanaanza leo kwenye mtandao wa Facebook yameamsha hasira za waislamu duniani. Nchini Pakistan mitandao ya Facebook na Youtube imefungiwa kwa muda.
Mashindano hayo yanayoitwa "Everybody Draw Muhammad Day" yanahamasisha watu duniani kushindana kuchora katuni za mtume Muhammad (s.a.w) kwa kupitia mtandao wa Facebook.

Mwanzilishi wa kampeni hiyo ya kuchora katuni za mtume msanii wa Marekani, Molly Norris alichora katuni za vitu mbalimbali kama vile viti, meza, pamba na vitu vingine kadhaa na kisha alisema vitu hivyo ndiyo katuni za mtume.

Mashindano hayo ambayo yaanza kwenye Facebook yameamsha hasira za waislamu kona mbalimbali duniani. Nchini Pakistan, mahakama imezifungia kwa muda tovuti za Facebook na YouTube mpaka mei 31 ambapo mashindano hayo yatakuwa yameishaisha.

Mamia ya watu waliandama katika mji mkuu wa Pakistan, Lahore kupinga mashindano hayo ambayo yameelezwa kuwa yana ukashifu uislamu.

Kwa mujibu wa Uislamu ni marufuku kuchora au kutoa picha yoyote na kudai kuwa ni ya mtume au inamwakilisha mtume.

Waanzilishi wa mashindano hayo kwenye Facebook walisema kuwa wameanzisha mashindano haya ili kuonyesha kuwa hawaogopi vitisho vya waislamu ambao hupenda kutoa vitisho kwa watu wanaochora katuni za mtume.

"Hawawezi kuchukua haki yetu ya uhuru wa kujieleza kwa kutulazimisha tukae kimya kwa sababu ya kuwaogopa", ilisema taarifa kwenye ukurasa wa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment