KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 13, 2010

Mahakamani kwa wizi wa Mil.6

ABROSE Joseph (20) mkazi wa Tabata Segerea na Mary Aloyce mkazi wa Mikocheni , wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa shilingi milioni 6.

WAtuhumiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Janeth Kanyage na kusomewa mashitaka na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Msaidizi wa Polisi, Musa Gumbo.

Gumbo alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Mei 3 mwaka huu .

Alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walipanga njama ya kumuibia mlalamikaji Kapuya katika eneo la Gongo la Mboto ambapo Abrose Joseph aliiba Euro 3,350 sawa na zaidi ya Shilingi milioni sita na kwenda kuzihifadhi kwa Mary Aloyce.

Gumbo alidai kuwa Abrose ni mfanyakazi wa ndani na baada ya kuziiba alipeleka fedha hizo kwaMary Mikocheni B ambaye alizipokea na kuzihifadhi huku akijua kuwa fedha hizo ni za wizi.


Washtakiwa hao walikana shtaka hilo na Mary yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye uwezo wa ku saini dhamana ya shilingi milioni 3 kila mmoja.

Hivyo Abrose alirudishwa rumande kwa kukosa , kesi hiyo itarudishwa tena Mei 25, mwaka huu kwa kutajwa.

No comments:

Post a Comment