KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, May 4, 2010

Maafisa wa usafiri wa anga nchini Ireland wamesema watapiga marufuku safari zote


Maafisa wa usafiri wa anga nchini Ireland wamesema watapiga marufuku safari zote za ndege zinazoingia au kutoka nchi hiyo. Hii ni kwa kwa sababu ya uwezekano wa hatari inayotokana na majivu ya volcano ambayo yanarushwa angani kutoka iceland.

Marufuku hiyo mpya itatekelezwa kuanzia saa 0700 hadi 1300 siku ya Jumanne.

Wasimamizi wa safari za anga nchini Ireland wamesema kuwa, viwango vya majivu kutoka kwa Volcano hiyo vinakadiriwa kuzidi vile vinavyokubalika kwa injini za ndege.

Safari za ndege kupitia Uingereza zilipigwa marufuku kwa siku sita mwezi uliopita kwa sababu ya hofu kuwa majivu ya volcano hiyo huenda yakawa na athari kwa injini za ndege.

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa shirika la safari za anga nchini Ireland (IAA) , Eamon Brennan, amesema ana matumaini kuwa hali hiyo itakwisha.

Uamuzi huo uliafikiwa baada ya kituo cha kutoa mawaidha kuhusu majivu ya Volcano (VACC) Kusema majivu hayo yalikuwa yanaelekea upande wa Ireland.

Lakini mkurugenzi mkuu wa IAA Eamon Brennan amesema ana imani kuwa vikwazo hivyo huenda vikaondolewa baadaye siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment