KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 20, 2010

Kortini kwa ubakaji

MKAZI mmoja jijini Dar es Salaam aitwae Dunia Macho (42), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jana, akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka minne.
Mshitakiwa huyo ambaye hati ya mashitaka ilionyesha ni fundi ujenzi alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Agnes Mchome wa mahakama hiyo.

Mwendesha Mashitaka, Inspekta Masaidizi wa Polisi, Naima Mwanga alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 11, mwaka huu, katika majira ya saa 11 jioni huko katika maeneo ya Pungu Mwakanga.

Mwanga alidai kuwa katka nyakati hizo mshtakiwa huyo alimuingilia kimwili mtoto huyo [jina kapuni] bila ridhaa yake na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.

Hata hivyo mshitakwia alikana shtaka hilo na alirudishwa rumande kwa kukosa dhamana, na kesi hiyo iliahirishwa na itarudi tena mahakamani hapo Juni Mosi, mwaka huu kwa kutajwa.

Wakati huohuo Ali Hamisi [28] amefikishwa katika Mahakama hiyo akikabiliwa na kosa ya kula njama na kupora mali ya shilingi laki tano.

Ilidawa kuwa mshitakwia huyo malitenda kosa hilo Mei 10, mawka huu huo maeneo ya Ialala ambapoo alitengeneza mazingira ya uporaji na kufanikisha adhma hiyo na kujinyakulia mali ya thamanai hiyo.

Nae alikana shtaka na alipelekwa rumande kwa kukosa mdhamini mmoja wa kumdhamini mahaka mani hapo.

No comments:

Post a Comment