KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 10, 2010

Jumuiya ya Ulaya kuinusuru Euro


Mawaziri wa fedha wa muungano wa bara Ulaya wamekubaliana mpango wa dharura wa euro bilioni 500 ili kuzuia kusambaa kwa matatizo ya deni la Ugiriki katika nchi nyingine.

Nchi 16 zinazotumia sarafu hiyo moja ya euro zitaweza kupata euro bilioni 440 kama dhamana ya mikopo na euro bilioni 60 za mfuko wa tume ya dharura ya Ulaya.

Shirika la fedha duniani (IMF) pia litachangia hadi euro bilioni 250.

Kamishna wa masuala ya uchumi Olli Rehn amesema makubaliano hayo yamethibitisha kuwa "tutalinda sarafu ya euro kwa vyovyote vile".

Kumekuwa na wasiwasi kwamba bila hatua hizo kuchukuliwa,sarafu ya euro ingeshuka thamani kwenye masoko huku wawekezaji wakiwa na wasiwasi na nchi zenye matatizo ya fedha kama vile Ureno na Uhispania.

No comments:

Post a Comment