KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

Gordon Brown kuondoka madarakani

Brown kuachia ngazi kama mwenyekiti wa Labour

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema anang'atuka kama kiongozi wa chama cha Labour.




Bw Brown amesema hayo huku chama chake kikianza rasmi mazungumzo na chama cha Liberal Democrats kuhusu kuunda serikali.

Bw Brown ambaye amekuwa waziri mkuu tangu mwaka 2007, amesema ana imani kuwa kiongozi mpya atapatikana ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Chama cha Lib Dem kimekuwa kikifanya mazungumzo na chama cha Conservative, ambacho kimeshinda viti zaidi kuliko chama kingine chochote katika uchaguzi wa Uingereza.

Hata hivyo chama cha Lib Dem kimetaka kuwepo na mazungumzo rasmi na chama cha Labour. Bw Brown amesema hatua waliyofikia ni kwa ajili ya "manufaa ya taifa".

David Cameron, Gordon Brown na Nick Clegg


Taarifa ya Bw Brown itaonekana kama hatua ya kuongoza njia ya kufikia makubaliano kati ya Labour na Liberal Democrats kuunda serikali.

Hatua hii imekuja baada ya wabunge wa Lib Dem kumtaka kiongozi wao Nick Clegg na wajumbe wake kuendelea kuzungumza na Labour, huku wakitafuta ufafanuzi katika masuala muhimu kutoka upande wa Conservative.

No comments:

Post a Comment