KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 20, 2010

Fabregas Kuitosa Arsenal, Kuhamia Barcelona


Mchezaji nyota wa Arsenal Cesc Fabregas ameamua kuitosa Arsenal na kuuomba uongozi wa Arsenal umruhusu arudi kwenye timu yake ya zamani ya Barcelona ya Hispania ambayo wiki hii imetuma maombi rasmi ya kumnunua Fabregas.
Jahazi la Arsenal linaonekana kuyumbayumba baada ya nahodha wake, Cesc Fabregas kuamua kushuka kwenye jahazi hilo kuanza safari ya kurudi kwao Hispania.

Fabregas ambaye alikuwa kimya muda mrefu wakati tetesi za kuhamia Barcelona zilipovumishwa, ameamua kuvunja ukimya na kuutaka uongozi wa Arsenal umpe ruhusa ahamie Barcelona.

Fabregas amezidi kumuumiza kichwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger baada ya kuweka wazi kuwa anataka suala lake la usajili lishugulikiwe mapema iwezekanavyo ili aende kwenye kombe la dunia kichwa chake kikiwa fresh hakina mawazo ya usajili.

Barcelona kwa upande wao wamesema wako tayari kuipa Arsenal kiungo wake Yaya Toure pamoja na dau watakalokubaliana.

Wakati huo huo Barcelona iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa nyota wa Valencia, David Villa ambaye kama mambo yakienda sawa siku ya alhamisi atatambulishwa rasmi mbele ya washabiki wa Barcelona.

No comments:

Post a Comment