KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 20, 2010

Boateng amuomba radhi Ballack

Kiungo wa Ghana Kevin Prince Boateng ameomba radhi kutokana na rafu aliyocheza iliyomfanya nahodha wa Ujerumani Michael Ballack kutoweza kucheza Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Ballack alijeruhiwa baada ya kukabiliwa na mchezaji huyo wa Portsmouth siku ya Jumamosi.


Boateng, ambaye atakuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachokabiliana na Ujerumani katika kundi D kwenye fainali za Kombe la Dunia, amesisitiza hakukusudia kumuumiza Ballack.

Boateng amesema "Naomba radhi. Sikukusudia kumuumiza. Ilikuwa ni tukio lililotokea bila kupanga."

Naomba radhi. Sikukusudia kumuumiza. Ilikuwa ni tukio lililotokea bila kupanga.
Kevin Prince-Boateng
"Ni tukio lililoonekana la kupuuzi, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alieleza kupitia gazeti la michezo la Bild la Ujerumani.

Msamaha huo umetolewa siku tatu baada ya Ballack kuchezewa rafu wakati wa fainali ya kuwania kombe la FA baina ya Portsmouth na klabu anayochezea na haujawapunguzia ghadhabu Wajerumani wanayoilekeza kwa Boateng.

Ballack aliumia katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo wa Jumamosi, baadae timu yake ilishinda bao 1-0.

Nafasi ya mwisho Ballack kucheza Kombe la Dunia

Mashabiki siku ya Jumanne waliporomosha hasira zao kupitia mitandao mbalimbali na wakamwita Boateng "adui namba moja wa Ujerumani" na kumeanzishwa mijadala kwenye mitandao, mmoja ukipewa jina la '82 million against Boateng' au 'Anti-Boateng Group', yote ni kuonesha hasira zao dhidi ya Boateng.

Boateng, aliyezaliwa Berlin baba yake ni Mghana na mama ni Mjerumani, hakuwa na uhusiano mzuri na mashabiki wa soka wa Ujerumani tangu akichezea Hertha Berlin.

Pia ana uhusiano wa mbali na mchezaji maarufu wa soka wa zamani wa Ujerumani, Helmut Rahn, aliyefunga bao la ushindi kwa Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1954 dhidi ya Hungary.

Boateng mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea pia Tottenham Hotspur, ataiwakilisha Ghana katika Kombe la Dunia, wakati kaka yake Jerome yumo katika kikosi cha awali cha Ujerumani kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia.

Kinachozidi kuweka mazingira magumu ya suala hilo ni kutokana na Ghana na Ujerumani kuwa kundi moja la D na watakwaruzana tarehe 23 mwezi wa Juni mjini Johannesburg.

Ballack, ambaye hatacheza fainali hizo, kama angecheza hizi zingekuwa fainali zake za tatu za Kombe la Dunia na kwa sasa yupo Sicily baada ya kipimo kuonesha ameumia kiwiko cha mguu hali itakayomfanya awe nje ya uwanja kwa wiki nane.

Siku ya Jumanne Ballack alisema hakuna haja ya kuwekeana uhasama.

"Kwa kweli nimekasirika sana na kukatishwa tamaa, lakini katika soka hayo yanatokea."

No comments:

Post a Comment