KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 20, 2010

Bidhaa bandia za Mil.43 zateketezwa

TUME ya ushindani ya biashara imeteketeza bidhaa bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43 ambazo hazikuwa sahihi kwa matumizi ya binadamu.

Bidhaa hizo ziliteketezwa jana katika dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaaam.

Mwanasheria wa Tume hiyo Bw. Elton Mhete amewataka wafanyabiashara wawe makini wanapoingiza bidhaa zao ndani ya nchi wahakiki kuwa ni sahihi na zinafaa kwa matumizi ya binadamu.

Aliusema pindi ikigundulika kuwa bidhaa hizo ni bandia tume hiyo zinateketeza moto kwa kuwa bidhaa hizo zikiachiwa wananchi wazitumie zina madhara makubwa kwa binadamu

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na Jenereta, Tv, wino wa computer, always, balbu zikiwemo na juice ambazo hazikuwa sahihi kwa matumizi ya binadamu.

No comments:

Post a Comment