KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 20, 2010

Ben Foster ajiunga na Birmingham


Klabu ya Birmingham imemsajili mlinda mlango Ben Foster kutoka Manchester United kwa mkataba wa miaka miwili, bila kutajwa kiwango cha pesa alichonunuliwa.

Foster ambaye alikuwa akidakia timu ya taifa ya England ataziba pengo la Joe Hart aliyerejea klabu yake ya Manchester City baada ya kumaliza kuichezea Birmingham kwa mkopo.

Foster alijiunga na Manchester United akitokea Stoke mwaka 2005 na mwezi wa Julai mwaka 2009 alisaini mkataba mnono wa miaka minne na klabu hiyo ya Old Trafford.

Msimu uliopita alianza akiwa mlinda mlango wa kwanza wa United lakini makosa aliyofanya wakati wa mechi ya kuwania Ngao ya Jamuia dhidi ya Chelsea halikadhalika mchezo dhidi ya Manchester City ulimfanya awekwe kando.

Mlinda mlango huyo mara ya mwisho kuichezea England ilikuwa mwezi Novemba mwaka 2009 dhidi ya Brazil, lakini kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa kiwango cha klabu kulimsababishia aondolewek timu ya taifa na zaidi ya hapo ameachwa katika kikosi cha England cha Kombe la Dunia, ambapo Joe Hart amechaguliwa.

Meneja wa United Sir Alex Ferguson tayari amekwishatangaza kumpandisha katika kikosi cha kwanza msimu ujao mlinda mlango wa timu ya taifa ya England ya chini ya umri wa miaka 21 Ben Amos akiwa nambari tatu kwa kipa namba moja Edwin van der Sar na yule nambari mbili Tomasz Kuszczak.

Ferguson amesema "Kwa sasa anakuwa mlinda mlango wetu wa tatu, ni kijana mwenye kipaji na ana maendeleo makubwa kuelekea siku za usoni."

No comments:

Post a Comment