KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 15, 2010

Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki limepitisha mapendekezo ya kuongezwa kwa mshahara

Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki limepitisha mapendekezo ya kuongezwa kwa mshahara wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa dola za Marekani 1,500 kutoka mshahara wa sasa wa dola 3,300 kwa mwezi na kuwa dola 4,800..

Hata hivyo, mapendekezo hayo ya Bunge hilo lenye wabunge 52 yatawasilishwa katika kikao cha wakuu wa nchi kwa ajili ya uamuzi wa mwisho

Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao maalum cha Baraza la Mawaziri la EAC kilichomalizika juzi mjini hapa ambacho pia kimependekeza bajeti ya matumizi kwa mwaka wa 2010/2011 ya dola za Marekani 59,963,040,

Bajeti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge la EAC mwezi ujao, kimelitengea Bunge hilo dola 1,047,892 ili kumudu ongezeko hilo la mishahara ya wabunge.

Kiasi cha dola za Marekani 29,141,051 zitatokana na nchi washirika na wahisani wa maendeleo wa jumuia hiyo wakati kiasi cha dola za 73,620 zitatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Baraza hilo pia limeeleza kuwa nchi wanachama zimeweza kukamilisha michango yake katika bajeti ya mwaka uliopita wa fedha wa 2009/2010 na hivi sasa zinajipanga kuanza kuwasilisha ya bajeti ijayo.

No comments:

Post a Comment