KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 20, 2010

Auawa na kutupwa kando ya barabara

KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Bakari amepoteza maisha kwa kuuawa kikatili na watu wasiojulikana na kumtupa pembezoni mwa barabara huko maeneo ya Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la mauaji lilitokea jana majira ya alfajiri, katika maeneo hayo ambapo maiti ya kijana huyo ilikutwa kando ya barabara katika majani ikiwa imefungwa kamba miguuuni na mikononi.

Kijana huyo ilidaiwa kuwa ni mwajiriwa na mkazi mmoja maeneo hayo ambapo ni dereva wa familia aliyeajiwa katika familia moja maeneo hayo.

Kijana huyo alivamiwa na wauaji hao na kumfunga kamba miguuuni na mikononi na kisha kumuua na wezi kuondoka na gari ndogo aliyokuwa akiendesha.

Ilidaiwa kuwa kijana huyo ni dereva wa familia moja katika maeneo hayo na kila alfajiri hufika katika nyumba hiyo kuwapeleka wanafunzi shuleni na wakati akielekea huko ndipo njiani wezi hao walimvizia na kumpora gari hilo na kumuua na kumtupa kando ya barabara.

Hata hivyo jeshi la polisi linafanya msako mkali kuwabaini watu waliohusika katika tukio hilo la mauaji.

No comments:

Post a Comment