KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 20, 2010

Aliyenusurika MV Bukoba achapisha kitabu


Nyaisa Simango ambaye ni miongoni mwa watu wachache walionusurika katika ajari ya Mv Bukoba iliyotokea siku ya Jumanne Mei 21 mwaka 1996 amezindua kitabu chake alicho kitunga kinachozungumuzia jinsi ajari hiyo ilivyotokea.
Nyaisa Simango ambaye ni miongini mwa watu wachache walionusurika katika ajari ya Mv Bukoba iliyotokea siku ya Jumanne Mei 21 mwaka 1996 amezindua kitabu chake alicho kitunga kinachozungumuzia jinsi ajari hiyo ilivyotokea.

Kitabu hicho kilichpewa kichwa cha habari isemayo "SITISAU MV BUKOBA" kina kurasa 167 zinazoeleza hali halisi ilivyokuwa ndani ya meli ya Mv Bukoba kabla na baada ya ajari , Nyaisa Simango ni miongoni mwa abiria wachache walionusurika katika ajari hiyo,amejaribu kuelezea tanga mwanzo wa safari yake kutoka Dar es Salaam kwa Train hadi mwanza, na kutoka mwanza kwenda Bukoba na safari yake ya kurudi kutoka bukoba na meli hiyo hadi ilipoishia kwa kupinduka na kuzama,

Kiasi cha maili kumi hivi kabla ya kufika bandarini Mwanza, amejaribu kuelezea matatizo mbalimbali ya Mv Bukoba tangu mwanzo mwa safari hadi kuzama kwake,na kinaelezea athari za ajari hiyo kijamii na kiuchumi na kisiasa katika kitabu hicho mwisho kinahitimisha kwa kutoa uchambuzi wa majanga kama haya pia katika kitabu hicho Nyaisa ametoa mabendekezo na ushauri katika taasisi mablimbali zinazo toa huduma kwa jamii.

Nyaisa Godfrey Simango alizaliwa katika Wilaya ya kinondoni jijini Dar es Salaam, alisoma elimu ya msingi na sekondari katika Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara kuanzia mwaka 1981 hadi mwaka 1991 alipata stashahada ya juu ya ubaharia katika chuo cha uongozi wa maendeleo, Mzumbe IDM-MZUMBE 1999 Aidha mwaka 2004 alihitimu shahada ya uthamili katika uongozi wa biashara ,mchipuo na fedha na benk (MBA- Finance and Banking ) chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro, kwa sasa Nyaisa Sumango ameajiriwa kama Afisa Ugavi katika Benki Kuu ya Tanzania,

Nyaisa alisema kuwa wakati anapata ajari hiyo,alikuwa ni mwajiriwa wa jeshi la Magereza katika kituo cha Ukonga jijini Dar es Salaam, ambapo katika safari hiyo alikuwa amepeleka mmoja wa wafungwa katika kesi yake huko mkoani Kagera.

Kitabu hicho kinasisimua sa ukikisoma kwa makini utagundua kuwa ajari hiyo ilitokana na ukosekanaji wa ulinzi kwa sekta husikia hata hivyo Nyamonga alisema alikuwa katika hoteli iliyopo katika meli hiyo akipata kinywaji pamoja na wenzaka lakini baadaye aliondoka kurudi kwenye chumba chake ,

Hivyo aliamua kwenda bafunu kuoga lakini akiwa huko aliona meli ikuyumba na kupinduka juu kukawa chini chini kukawa juu, hivy0 alipoteza ramani ya mle chumbani kwani ilikuwa mala yake ya kwanza kupanda meli katika maisha yake alikuwa hajawahi,mkupanda meli.

Kitabu hicho CHA SITASAHAU MV BUKOBA kwa sasa kinapatikana katika maduka mbalimbali yanayouza vitabu nchini Tanzania na kila nakala itauzwa shilingi 12,000. na kwa hatua hii ya kwanza amechapisha nakala 2000, kampuni iliyochapa kitabu hicho ni Vision Puplishing Limited .

No comments:

Post a Comment