KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, December 27, 2009

LINDA UHAI WAKO MAISHANI

Maisha ya ndoa ni zawadi kutoka kwa mwenyezi mungu maishani

Kenya yafuta Polisi 88





Taarifa kutoka Kenya zinasema serikali imewafuta kazi maafisa 88 wa Polisi kwa kukiuka taratibu za serikali.

Radio ya shirika la utangazaji la Kenya KBC imemnukuu afisa wa ngazi za juu katika Polisi Bwana Kinuthia Mbugua , akisema uamuzi huo umechukulia ili kurekebisha hadhi ya kikosi cha Polisi na kuwapa watu imani.

Bwana Mbugua ameripotiwa kusema kwamba umma umepoteza imani na Polisi kutokana na tabia ya maafisa wanaokiuka sheria.


Amesema wakuu wa Polisi wanajaribu kwa kila njia kurejesha heshima ya kikosi cha Polisi nchini Kenya.

Waisrael wauwa Wapalestina sita


Hiki ni kizazi cha baba wetu wa imani kinachopambana wenyewe kwa wenyewe kwa msaada wa nchi za magharibi na marekani.
mpaka sasa Tatizo la kizazi cha wana Wa Nabii Ibrahimu limekuwa janga na maslahi kwa baadhi ya watu Duniani.

Kizazi cha Israel au nabii Jakubu ndicho kizazi Kinachotokana na Mtoto wa Pili wa Ibrahimu ambae ni Isihaka (Isack) na kizazi cha Warabu kinatokana na mtoto wakwanza wa Nabii Ibrahimu, ambae ni Ismail.

Tatizo la wapalestina na waisrael lina misingi miwili mikubwa duniani, ambayo ni Dini na Siasa katika umiliki wa ardhi.

Waisrael wauwa Wapalestina sita

Wanajeshi wa Israeli wamewauwa Wapalestina sita, watatu katika ukanda wa Gaza na wengine watatu katika Ukingo wa Magharibi.

Msemaji wa Israel ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kuwa Wapalestina watatu waliouwawa Gaza ni kutokana na shambulio la anga.


Katika Ukingo wa Magharibi, wanajeshi wa Israel wanaarifiwa kuwapiga risasi na kuwauwa Wapalestina watatu katika mji wa Nablus.


Mashambulio hayo yametokea siku mbili baada ya raia mmoja wa Israel kuuwawa katika shambulio la kuvizia katika Ukingo wa Magharibi.

Baba wa kijana ambaye alitaka kulipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria karibu 300,


Baba wa kijana ambaye alitaka kulipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria karibu 300, alionya Marekani kuhusu vitendo vya mwanawe na hasa msimamo wake mkali wa kisiasa.
Babake mzazi, Alhaji Umaru Mutallab, ambaye ni mfanyibiashara maarufu nchini Nigeria alikuwa ametoa ripoti kwa ubalonzi wa Marekani jijini Abuja.

Mnamo michache iliyopita alielezea wasiwasi wake kuhusu msimamo mkali wa kisiasa wa mtoto wake ambaye anasomea uhandisi kwenye chuo kikuu kimoja mjini London, University College London.

Kutokana na jaribio hilo mnamo siku ya Krismasi, usalama umeimarishwa katika viwanja mbalimbali duniani kote.

Maswali mazito

Kijana huyo amefunguliwa mashtaka akiwa hospitalini Michigan ambako amelazwa na majeraha ya mguu aliyopata alipojaribu kuwasha mabomu ambayo alikuwa amejifunga mwilini na kwenye suruali yake ya ndani.

Wakati akijaribu kujilipua, abiria wenzake na wahudumu wa ndege walimwandama kwa nguvu huku ndege hiyo iliyokuwa imesafiri kutoka Uholanzi ikijiandaa kutua mjini Detroit, Marekani.

Familia ya kijana huyo pia iliilezea Idhaa ya Hausa ya BBC kwamba hawakuwa tena na mawasiliano na mtoto wao tangu mwezi Oktoba alipokuwa akiishi Yemen.

Inaripotiwa kwamba aliondoka Yemen akaelekea Ethiopia, halafu Ghana na kisha Nigeria.

Bado kuna maswali mazito kuhusu jinsi Mutallab ambaye ana Visa halisi ya kusafiri hadi Marekani, alivyopanda ndege kutoka Lagos hadi Amsterdam licha ya kuwepo na taarifa kuhusu vitendo na mienendo yake.

Tuesday, December 8, 2009

Mgomo wa Daladala wazua kashehe Tz


Mgomo wa Daladala wazua kashehe Tz

Madereva wa mabasi zaidi ya tisini yanayotoa huduma ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam, nchini Tanzania hii leo wanakabiliwa na hatua za kisheria kutokana na mgomo wa jana wa kusitisha huduma hiyo.
Mgomo huo unafuatia operesheni inayoendeshwa kwa pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu, SUMATRA, jeshi la polisi na kampuni ya uwakala ya Majembe Auction Mart katika kukabiliana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Madereva wa mabasi hayo maarufu kama DALADALA wanasema faini za sasa ni kubwa mno ikilinganishwa na walivyokuwa wakitozwa kati ya dola ishirini na thelathini za Kimarekani kabla ya operesheni hiyo.

Shambulio la bomu laua 118 Baghdad


Shambulio la bomu laua 118 Baghdad

Taarifa kutoka Iraq, zinaeleza kuwa watu zaidi ya 118 wameuawa katika mashambulio ya mabomu mjini Baghdad.
Inaarifiwa kuwa mabomu hayo yalikuwa yametegwa ndani ya magari yaliyokuwa yameegeshwa maeneo tofauti.

Mabomu hayo manne yalilipuka kwa wakati mmoja, la kwanza likilipuka karibu na kituo cha polisi eneo la Doura lenye waisilamu wengi wa Sunni.

Wenye kufanya mashambulizi hayo wanasemekana walilenga hasa ofisi za serikali au vyuo vikuu.

Wizara ya mambo ya ndani ni miongoni mwa majengo yaliyoshambuliwa. Hakuna aliyekiri kutega mabomu hayo.

MSINGI WA MAPENZI MAISHANI NI MANENO MA MATENDO VIZURI

KILA JAMBO MAISHANI LINAHITAJI USHIRIKIANO WA UPENDO

Ntaganda akanusha kushirikiana na FLEC


Ntaganda akanusha kushirikiana na FLEC

Huku maafa yakiendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda amekana madai ya kushirikiana na kundi jingine la waasi.
Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inasema kundi linaloongozwa na Bosco Ntaganda linalowasaka waasi wa FDLR huenda likawa tishio kubwa mashariki mwa Congo.

Bosco Ntaganda amekanusha madai ya umoja wa mataifa kuwa, anashirikiana na kundi la waasi lijulikanalo kama Front for the Liberation and Emancipation of the Congo (FLEC).

Bw Ntaganda amekanusha madai hayo katika mahojiano aliyofanya na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.


Wafungwa Burundi wafanya ghasia


Wafungwa Burundi wafanya ghasia

Wafungwa katika gereza kubwa zaidi la Burundi wamefanya ghasia wakilalamikia walichotaja kama hali mbaya ya maisha na msongamano, huku wakitaka kundi fulani la wafungwa waachiliwe.
Baadhi ya wafungwa walivunja na kuondoka katika gereza la Mpimba nje ya mji mkuu wa Bujumbura kabla ya maafisa wa polisi kuwathibiti.

Mapema moto uliowashwa na wafungwa hao uliteketeza mafaili ya wafungwa.

Mkereketwa wa haki za kibinadamu, Pierre Mbonimpa, alisema wafungwa walikuwa wakilalamikia hali mbaya zinazokiuka haki za kibinadamu na walitaka kuachiliwa mapema wa wafungwa wakisiasa, wazee na watoto.



Gereza la Mpimba lilijengewa wafungwa 800 lakini kwa sasa lina wafungwa 3,500

Maandamano Sudan kupinga Serikali




Waandamanaji nchini Sudan wameteketeza afisi za chama cha rais Omar Al Bashir zilizoko mji wa kusini kulalamikia kukamatwa kwa viongozi watatu wa chama cha SPLM.
Hakuna taarifa kuhusu waathirika katika majengo ya chama cha National Congress mjini Wau. Baadaye polisi waliwaachia huru wanasiasa hao.

Chama cha SPLM kilijiunga na serikali mwaka wa 2005 na kumaliza vita kati ya eneo la Kusini na Kaskazini.

Hata hivyo taharuki kati ya SPLM na washirika wao serikalini kutoka chama cha NCP imeendelea huku uchaguzi mkuu ukikaribia hapo mwakani.

Huu ndio uchaguzi mkuu wa kwanza kwa miaka 24 ambapo raia watamchagua rais, wabunge na wakuu wa mabaraza.