KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 20 tangu ulipoangushwa ukuta wa Berlin


Viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 20 tangu ulipoangushwa ukuta wa Berlin, wamesema harakati dhidi ya madhila sehemu mbalimbali duniani hazina budi kuendelezwa.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wakati wa maadhimisho hayo kwenye lango la Brandenburg alijumuika na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Waziri wa Mammbo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.

Viongozi hao wameonya mamilioni ya watu duniani bado wanaedelea wanavunjiwa haki zao za kibinadamu.

Ukuta wa Berlin uliangushwa mwaka 1989 hali iliyosababisha Ujerumani kuungana upya na ndio chanzo cha kuanguka kwa Muungano wa nchi za Urusi na kumaliza vita baridi.

Ujerumani Mashariki iliyokuwa ya Kikomunisti ilijenga ukuta huo wa kilometa 155 mwaka 1961 ikijitenga na Berlin Magharibi hali iliyowazuia raia wake kutorokea magharibi kukimbia siasa za Kikomunisti.

Bi Merkel aliyekulia Ujerumani Mashariki, katika sherehe hizo aliongoza maandamano yaliyopita lango la Brandenburg lililo ishara ya kuunganika upya kwa Ujerumani mwaka 1990

No comments:

Post a Comment